Deuteronomy 11:9-12

9 aili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayo Bwana aliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali. 10 bNchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga. 11 cLakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni. 12 dNi nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

Copyright information for SwhKC